Rwanda yaadhimisha siku ya watoto duniani na kutoa wito wa kukomesha unyanyasaji wa kifamilia
2024-11-21 08:50:08| CRI

Rwanda imeungana na jumuiya ya kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Watoto Duniani, ikiwa na wito wa kukomesha unyanyasaji wa kifamilia, unaoendelea kutishia haki za watoto.

Kwenye sherehe hizo zilizofanyika mjini Kigali, mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Mtoto la Rwanda (NCDA) Assumpta Ingabire amesema kuwa kulea mtoto ni jukumu lisiloweza kubadilishwa. Ili kuhakikisha ukuaji na maendeleo yao sahihi, lazima watengenezewe mazingira yatakayowawezesha kustawi na kukua na kuwa raia wema. Lazima wakomeshe unyanyasaji wa kifamilia.

Amesisitiza masuala muhimu yanayoathiri watoto, ikiwa ni pamoja na kudumaa kwa watoto na unyanyasaji wa majumbani, ambao mara nyingi yanawalazimisha watoto kuingia mitaani. Pia amesisitiza umuhimu wa kulea watoto kwa kuwajibika katika kutatua changamoto hizo.