Mwanariadha wa Jeshi la Polisi la Tanzania Konstebo Transfora Mussa ameshinda mbio za kilomita 10 za Fulham zilizofanyika Uingereza huku akivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa kwa kukimbia muda mfupi zaidi.
Kontebo Transfora ambaye amepata medali ya dhahabu, amevunja rekodi hiyo kwa kutumia dakika 31:53 tofauti na rekodi iliyowekwa mwaka 2023 na mwanariadha kutoka Kenya aliyeshinda kwa kutumia dakika 33:11 katika mashindano hayo.
Konstebo Transfora amesema nidhamu pamoja na maandalizi mazuri aliyoyafanya ndio msingi wa mafanikio hayo ambapo ameahidi kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine.