Uchunguzi uliofanywa na Shirika la Ujerumani la Washauri Bingwa la Bertelsmann Stiftung Jumatano umeonyesha kuwa, watu wengi wa Ulaya wanaona kuwa chini ya hali ya sasa ya siasa za kijiografia, Ulaya inapaswa kutafuta njia ya kuwa huru zaidi badala ya kuitegemea Marekani.
Uchunguzi huo uliofanywa katika nchi wanachama wote 27 wa Umoja wa Ulaya na Marekani umeonyesha kuwa, asilimia 63 ya washiriki wanaamini muda umefika sasa kwa Ulaya kufuata njia yake, idadi ambayo imeongezeka sana ikilinganishwa na asilimia 25 ya mwaka 2017. Mbali na hayo, asilimia 73 ya watu wa Ulaya wanataka Umoja wa Ulaya ubebe jukumu zaidi katika mambo ya dunia ili kulinda maslahi yake katika utaratibu wa dunia unaobadilika.
Hata hivyo, watu wa Ulaya bado wanathamini ushirikiano wao na Marekani, hasa katika sekta ya usalama.