Wabrazil wanatarajia kuwa uhusiano kati ya nchi yao na China kuzinufaisha nchi za Kusini
2024-11-21 14:47:49| cri

Wananchi wa Brazil wanaona kuwa uhusiano kati ya China na Brazil ni uhusiano muhimu kati ya nchi za Kusini, na una mchango muhimu kwenye mambo ya usimamizi wa dunia.

Uchunguzi uliofanywa na Televisheni ya China CGTN kwa wahojiwa 1,106 wa Brazil, unaonyesha kuwa wahojiwa wanaamini kuwa uhusiano kati ya China na Brazil umevuka mipaka ya kuzinufaisha nchi hizo mbili tu, na sasa una manufaa kwa utaratibu wa ya pande nyingi duniani, umeongeza msukumo katika kulinda maslahi ya nchi za kusini, na kujenga utaratibu wa kimataifa wa haki zaidi.

Wakati China na Brazil zinaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati yao, utafiti huo pia umegundua kuwa wabrazil wana mtazamo chanya kuhusu China, asilimia 91.6 ya waliohojiwa wanaamini kuwa China ni nchi yenye mafanikio, na asilimia 84.5 wanaamini kuwa China ni nchi inayostahili kuheshimiwa.