Serikali ya Zimbabwe imetaka uwekezaji zaidi wa China katika sekta ya nishati nchini humo wakati ikikabiliwa na changamoto kubwa ya ugavi wa umeme.
Katika Jukwaa la Biashara kati ya Zimbabwe na China lililofanyika mjini Harare, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Umeme nchini humo, Edgar Moyo amesema, sekta ya nishati nchini Zimbabwe inatoa fursa zaidi za uwekezaji kutoka China, hususan chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, (BRI).
Bw. Moyo amesisitiza umuhimu wa China katika kutengeneza hatma ya sekta ya nishati nchini Zimbabwe, na kuipongeza nchi hiyo kwa kuunga mkono bila kusita na uratibu katika maendeleo ya nishati na umeme nchini humo katika miaka iliyopita.