• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makaburi ya wafalme wa Xixia na michoro ya mawe kwenye Mlima Helan

    (GMT+08:00) 2009-06-30 14:39:37

    Katika kipindi hiki cha leo, tutawafahamisha kuhusu historia na utamaduni wa enzi ya Xixia, makaburi ya wafalme na michoro iliyochorwa kwenye mawe ya Mlima Helan.

    Yinchuan, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia ulioko sehemu ya kaskazini magharibi ya China, unaitwa kwa jina zuri la "Mji wa Phoenix" toka zamani. Mji huu uko kwenye upande wa mashariki wa Mlima Helan, rasilimali kubwa ya utalii yakiwemo mabaki mengi ya historia ya enzi ya Xixia ya huko, vinawavutia watu wengi katika miaka ya karibuni.

    Katika muda wa kiasi cha miaka 200 kuanzia mwanzoni mwa karne ya 11 hadi mwanzoni mwa karne ya 13, tawi moja lililoitwa Dangxiang la kabila la Waqing, ambao ni wafugaji waliokuwa kwenye sehemu ya kaskazini magharibi mwa China katika zama za kale, waliasisi enzi ya kifalme ya Xixia kwenye sehemu ya kaskazini magharibi ya China, ambayo ni mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui la Ningxia kwa hivi sasa. Wakati ule enzi ya Xixia ilikuwepo nchini China pamoja na enzi nyingine mbili za kifalme za Jin na Song ya kusini. Baada ya miaka 200 hivi, enzi ya Xixia iliangamizwa na jeshi la Mongolia, na kuungana na kabila la Wahan na makabila mengine ya China.

    Ni mwendo wa nusu saa kwa gari kufika kwenye makaburi ya wafalme wa Xixia. Makaburi ya wafalme wa Xixia, ambayo ni moja ya maeneo makubwa ya makaburi ya wafalme yanayohifadhiwa vizuri hadi sasa nchini China, yanasifiwa kama ni "Piramidi ya mashariki".


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako