Makaburi ya wafalme wa Xixia yaligunduliwa katika miaka ya 70 ya karne iliyopita. Mwezi Juni mwaka 1972, kikosi kimoja cha sehemu ya jeshi ya Lanzhou kilikuwa kinajenga uwanja wa ndege wa kijeshi karibu na Mlima Helan, askari walipochimba msingi wa njia ya kurukia ndege waliona vitu vya udongo wa mfinyanzi vya zamani zaidi ya kumi pamoja na matofali kadhaa. Kutokana na kuelekezwa na watafiti wa mambo ya kale, waliendelea kuchimba, na hatimaye waligundua kaburi moja lililojengwa chini ya ardhi.
Licha ya kuona michoro iliyochorwa kwenye kuta za ndani za kaburi hilo, vilichimbuliwa baadhi ya vitu vya sanaa ya kazi za mikono, vitu vya sanaa ya ufinyanzi na matofali yenye maandishi na nakshi nzuri, watafiti wa mambo ya kale baada ya kufanya uchunguzi kwa makini, walithibitisha kuwa kaburi hilo ni la kipindi cha Xixia ya kale.
Katika muda wa karibu miaka 30 baadaye, watafiti walifanya uchunguzi kuhusu makaburi ya wafalme wa Xixia kwenye sehemu ya porini, waligundua kaburi moja la mfalme, makaburi manne ya watu waliozikwa wakiwa hai baada ya kifo cha mfalme, vibanda vinne vyenye mawe yenye maandishi ya kumbukumbu na mabaki ya jengo la Xia, ambapo waliona baadhi ya vitu vya kiutamaduni vya Xixia vikiwa ni pamoja na maneno ya enzi ya Xixia, michoro inayoonesha maisha ya wafugaji na wakazi wa mjini wa wakati ule, sanamu za aina mbalimbali, sarafu zilizotumika, vyombo vya shaba na kete za chesi za udongo wa mfinyanzi. Vitu vya kushangaza zaidi ni kuwa zilichimbuliwa sanamu nyingi za mawe na udongo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |