Baada ya kuwafahamisha kuhusu makaburi ya wafalme wa Xixia, sasa tunawafahamisha kuhusu michoro iliyochorwa kwenye mawe ya Mlima Helan.
Michoro hiyo mingi iko kwenye umbali wa zaidi ya kilomita 50 kutoka mji wa Yinchuan, michoro zaidi ya 1,000 ilichorwa kwenye mawe ya mitelemko ya milima ya eneo la zaidi ya mita 600 kando mbili za bonde kubwa. Michoro yake mingi ni ya vichwa vya binadamu, ambayo inachukua zaidi ya nusu ya jumla ya idadi ya michoro hiyo, ikifuatiwa na michoro ya wanyama wa ng'ombe, farasi, Punda, swala, ndege na mbwa mwitu. Mtafiti wa kituo cha utafiti wa michoro iliyochorwa kwenye mawe cha chuo kikuu cha makabila cha kaskazini Bw. Li Xiangsheng alisema,
"michoro mingi iliyoko kwenye sehemu ya kaskazini ni ya kuchongwa kwenye mawe, na mingine ni ya kuchorwa, na karibu michoro yote iliyoko kwenye sehemu ya kusini ni ya kuchorwa kwenye mawe, kwa mfano rangi iliyotumika katika michoro ya mawe ni iron oxide iliyochanganywa na damu ya ng'ombe, tena mitindo ya uchoraji ni ya aina mbalimbali"
Mwaka 1997 michoro iliyoko kwenye mawe ya Mlima Helan iliidhinishwa kuingia katika orodha ya mabaki yasiyo rasmi ya utamaduni wa dunia, mwezi Aprili mwaka 2004 michoro hiyo ilitolewa ombi rasmi la kuorodheshwa kuwa mabaki ya utamaduni wa dunia, na jumba la makumbusho ya michoro ya mawe ya Mlima Helan lilifunguliwa rasmi kwa watu.
Hivi sasa sehemu hiyo imekuwa "mji wa sinema na video wa magharibi mwa China". Filamu zaidi ya 60 zilipigwa huko.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |