• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makaburi ya wafalme wa Xixia na michoro ya mawe kwenye Mlima Helan

    (GMT+08:00) 2009-06-30 14:39:37

    Mkuu wa taasisi ya utafiti wa utamaduni wa Xixia Bw. Du Jianlu alisema, makaburi ya wafalme wa enzi ya Xixia ni lulu ya utamaduni iliyoko chini ya Mlima Helan. Alisema,

    "Makaburi ya wafalme wa Xixia yako kwenye eneo la karibu kilomita za mraba 50, kuna makaburi 9 ya wafalme na makaburi zaidi ya 100 ya watu waliozikiwa baada ya vifo vya wafalme."

    Mtafiti wa taasisi ya utafiti wa vitu vya utamaduni wa Xixia Bw. Niu Dasheng, hata leo hawezi kusahau jinsi alivyoshangaa siku ya kwanza alipoona makaburi ya wafalme wa Xixia, anasema.

    "Niliona makaburi makubwa sana, porini kabisa, mambo mengi yasiyofahamika…….hata ninashindwa kueleza, sijui mambo yaliyoko ndani yake, ni makaburi mengi hata nilishindwa kuona mwisho wake……"

    Kaburi la mfalme No. 3 lenye eneo la mita za mraba laki 1.5 ni kaburi kubwa, ambalo limehifadhiwa vizuri zaidi kati ya makaburi 9 ya wafalme wa Xixia, watafiti wamethibitisha kuwa kaburi hilo ni "kaburi la Tai" la mfalme mwanzilishi wa enzi ya Xixia. Mkuu wa idara ya taasisi ya utafiti wa utamaduni wa Xixia Bw. Du Jianlu anaona ugunduzi na utafiti kuhusu makaburi hayo ya wafalme ni muhimu sana. Alisema,

    "Makaburi ya wafalme wa Xixia ni makaburi ya kipekee ya makabila madogomadogo, mbali na makaburi ya wafalme ya enzi ya Qing katika utaratibu wa makaburi wa China. Kwa hiyo ni makaburi muhimu sana kwa utafiti wa utaratibu wa makaburi wa China. Mbali na hayo, vifaa vya ujenzi, hususan vifaa vya ujenzi wa majengo vinavyog'ara kama kioo ni muhimu sana kwa utafiti kuhusu historia ya ujenzi wa majengo. Ng'ombe wa shaba aliyegunduliwa vilevile ni muhimu sana kwa utafiti kuhusu kazi za mikono na teknolojia ya kusubu ya Xixia."


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako