• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maporomoko ya maji huko Hukou ya Mto Manjano

    (GMT+08:00) 2009-07-06 16:24:08

    Mto Manjano, ambao unaitwa "mto mama" wa China, unaonekana kama dragon mkubwa anayeruka angani. Mto huo unapita kwenye bonde kubwa la Qinjin lililoko katika uwanda wa juu wa udongo manjano wa sehemu ya kaskazini magharibi ya China, maji yake yanapopita kwenye sehemu ya Hukou mkoani Shanxi, yanapita kwenye sehemu finyu yenye upana wa kiasi cha mita 40 kutoka sehemu yenye upana wa kiasi cha mita 400, na kuleta kundi kubwa la maporomoko ya maji yenye umbo la kama kwato za farasi, hayo ndiyo maporomoko maarufu ya Hukou.
    Eneo la maporomoko ya maji ya Hukou ni kiasi cha mita za mraba 100, poromoko kubwa zaidi ni lenye upana wa mita 40, ambalo maji yanaanguka chini kutoka sehemu ya juu yenye kimo cha zaidi ya mita 30, ngurumo ya poromoko la maji inasikika kutoka mbali. Pamoja na kuwadia kwa likizo ya majira ya joto, shughuli za utalii kwenye sehemu mbalimbali zenye mandhari nzuri zinaanza kuongezeka kwa haraka, kivutio cha maporomoko ya maji ya Hukou pia kinawavutia watalii wengi wa nchini na wa nchi za nje.
    Maji ya Mto Manjano yanapofika kwenye sehemu ya Hukou, mto ukawa finyu kama mdomo wa birika kwa kubanwa na magenge ya mawe yaliyoko kwenye kando mbili za mto, hivyo inaitwa kuwa "hukou", maana yake ni "mdomo wa birika". Kabla ya kuingia kwenye sehemu ya poromoko la maji, ngurumo kubwa inasikika kutoka mbali.
    Maji ya mto yanaanguka chini moja kwa moja kutoka sehemu ya juu yenye kimo cha kiasi cha mita 30, wakati maji ya mto yanapokuwa mengi, upana wa poromoko la maji unazidi mita 1000. Maji ya mto yanayoanguka chini yanasababisha mawimbi makubwa, na matone ya maji yanavyorushwa yanaenea kwenye hewa kama ukungu mkubwa, jinsi ilivyo ni kama moshi unaotoka chini ya maji.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako