• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maporomoko ya maji huko Hukou ya Mto Manjano

    (GMT+08:00) 2009-07-06 16:24:08


    Kwa kuwa kiasi cha maji ya mtoni ni tofauti katika majira mbalimbali, mandhari ya sehemu ya Hukou vilevile yanabadilika, na yanakuwa mazuri zaidi katika vipindi viwili, kipindi cha kwanza ni katika mwezi Aprili na Mei ya majira ya Spring, ambapo maua ya mipichi ya mlimani yanachanua vizuri; kipindi cha pili ni katika majira ya kupukutika kwa majani kati ya mwezi Septemba na Novemba, wakati ule ni mwisho wa masika, maji ya vijito vya mlimani yanaingia kwenye mto, wakati upepo mwororo unapovuma, mara kwa mara upinde wa mvua unatokea angani. Katika vipindi hivi viwili, maji ya mto yanakuwa mengi, upana wa poromoko la maji unaweza kuzidi mita 1000.
    Katika majira ya baridi, poromoko la maji huwa linafunikwa na rangi nyeupe, kwenye magenge ya mawe karibu na poromoko la maji ni vipande vikubwa na vidogo vya barafu, na vinang'ara chini ya mwanga wa jua. Bila kujali kama kuna mawimbi makubwa au ni maji shwari, poromoko la maji la Hukou ni la kupendeza na kuvutia. Dada Xue kutoka mji wa Xian alisema,
    "Naona maporomoko ya maji ni mazuri sana, tena ni mazuri zaidi kuliko nilivyotarajia. Mawimbi yake naona ni makubwa zaidi kuliko ya mto Changjiang."
    Maji ya Mto Manjano yanatumiwa na wakazi wapole, wachangamfu na wenye bidii ya kazi wa sehemu ya kaskazini ya mkoa wa Shanxi. Nyimbo za kieneyeji zinasikika mara kwa mara kwenye uwanja wa juu wa udongo manjano, na watu wanaweza kuona mapambo ya kisanaa ya picha za karatasi zilizokatwa kwa mkasi kwenye madirisha ya nyumba za mapango ya udongo. Kama ukiwa na bahati, unaweza kuona maonesho ya ngoma ya Ansai ya wakazi wa huko kwenye sehemu zenye mandhari nzuri.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako