Hadithi hii inasema, zamani za kale kulikuwa na mkuu wa mkoa aliyepata uhamisho wa kwenda katika mji mkuu, alikwenda kwenye mtiririko wa chini wa Mto Manjano akiwa kwenye mashua. Mashua ilipofika kwenye mlima wa mlango wa Meng, giza lilianza kuingia, na mashua ikatia nanga. Usiku ofisa huyu alishuka kwenye mashua na kupanda mlima wa mlango wa Meng, na kuangalia mandhari ya usiku ya kisiwa hicho kilichoko kwenye Mto Manjano, aliona mwezi angani na mwezi ulioonekana kwenye maji ya mto, hali hii yenye mwezi wa kweli na mwezi usio wa kweli ilimvutia sana, akabuni maneno murua ya shairi ya "Mlima unayumbayumba kwa kufuata mawimbi, mawimbi yanayumbayumba katika mbalamwezi". Alirudi na kulala kwenye mashua, katika ndoto yake aliona mwezi ukiingia kwenye mashua. Asubuhi ya siku ya pili, wenzake walifafanua maana ya ndoto yake, na kusema, mlango wa Meng ni sehemu ya mwanzo ya mlango wa dragon, katika ndoto yake mwezi uliingia kwenye mashua, hii ni ishara nzuri kulingana na kauli ya "samaki wa lei akiruka mlango wa dragon".
Hapo baadaye mambo yalikuwa kama walivyosema, ofisa huyu wa mkoa alipandishwa cheo. Maneno manne makubwa ya rangi nyekundu yenye ukubwa wa mita za mraba moja kila neno moja ya "kulinda mkondo mkubwa wa maji", yaliyochongwa kwenye jiwe kubwa la mlango wa Meng yaliandikwa na huyo ofisa. Hivi sasa maji ya mto yanapokuwa machache, maneno hayo manne yanajitokeza juu ya maji, na yanawavutia watu wengi. Tokea hapo watu wakaita mlima wa mlango wa Meng kuwa mlima Mengmeng, maana yake ni mlima wa ndoto katika lugha ya Kichina.
Sehemu nyingine zenye mandhari nzuri kwa kufuata mtiririko wa maji ya mto huu ni pamoja na "ng'ombe wa jiwe kubwa anayelinda mto", magati ya enzi za Ming na Qing, mahali pa kuweka mizinga katika zama za kale na mtelemko wa Mlima Kenan, ambao maana yake ni mtelemko wa kuondokana na maafa.
Ili kuendeleza shughuli za utalii za sehemu ya Hukou, idara ya utalii ya huko inaanzisha mchezo wa magari kuzunguka kwenye sehemu hiyo ili kuvutia watalii wengi zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |