• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maporomoko ya maji huko Hukou ya Mto Manjano

    (GMT+08:00) 2009-07-06 16:24:08


    Mzee Zhang mwenye umri wa miaka 58, anajitokeza mara kwa mara kwenye sehemu ya poromoko la maji la Hukou. Mzee huyu anapenda kufunga kitambaa cheupe kichwani, kuvaa kizibau cha ngozi ya kondoo na kushika mkononi kamba inayomfunga Punda, akitoa huduma ya kupiga picha pamoja na watalii. Wakati mwingine anaimba nyimbo za kienyeji zinazoitwa Xintianyou kwa ajili ya watalii.
    Mzee Zhang alisema, hivi sasa maji ya maporomoko ya Hukou si mengi wala si machache, ikiwa ni wakati maji yanapokuwa mengi, watu hawaruhusiwi kusogelea maporomoko ya maji kwa kuhofia kuhatarisha usalama wao, ila tu wanaruhusiwa kuangalia maji kutoka mbali.
    Katika mapumziko ya siku ya wafanyakazi ya mwaka huu, idadi ya watalii waliotembelea maporomoko ya maji ya Hukou ilikuwa kubwa zaidi, ambapo sekta ya utalii iliuletea mji wa Yanan pato la Yuan milioni 250.
    Mbali na maporomoko ya maji, sehemu ya Hukou ina vivutio vingine. Si mbali kwenda kwa upande wa kusini ni mlango wa Meng, ambao ni mlango wa mwanzo wa kivutio cha mlango wa dragon. Hadithi moja ya kale inasema, samaki wa lei wa Mto Manjano akiruka mlango wa dragon, atabadilika kuwa dragon, kauli hiyo ni mfano wa mtu aliyepandishwa cheo na kuwa ofisa.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako