• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 8-Oktoba 14)

    (GMT+08:00) 2016-10-14 20:39:49

    Mfalme wa Thailand Bhumibol Adulyadej afariki

    Mfalme wa Thailand Bhumibol Adulyadej amefariki wiki hii akiwa na umri wa miaka 88. Taarifa iliyotolewa na jumba la kifalme la nchi hiyo imesema, mfalme Bhumibol Adulyadej alifariki katika Hospitali ya Siriraj huko Bangkok.

    Mfalme huyo aliingia madarakani alipokuwa na umri wa miaka 19, na ni mfalme aliyekuwa madarakani kwa muda mrefu zaidi duniani.

    Waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Prayut Chan-o-cha amesema, mwana mfalme Vajiralongkorn amewataka wananchi wote kuomboleza kifo cha mfalme kwa mwaka mmoja, na atarithi ufalme katika wakati mwafaka.

    Raia wa Thailand wameanza kuomboleza kufuatia kifo cha Mfalme Bhumibol , ambaye alikuwa nguzo ya uthabiti wa kisiasa nchini humo wakati wa utawala wake uliodumu miaka 70.

    Umati mkubwa wa waombolezai walikesha Bangkok wakiwa wamevalia mavazi ya rangi nyeusi, na wengi sasa wanarejea katika barabara za mji.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako