• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 8-Oktoba 14)

    (GMT+08:00) 2016-10-14 20:39:49

    Wasichana 21 wa Chibok waachiliwa Nigeria

    Maafisa wa serikali nchini Nigeria wanasema wasichana 21 wa shule ya Chibok ambao ni miongoni mwa wale waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram sasa wako huru na kwa sasa wamo mikononi mwa maafisa wa usalama katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

    Aidha imebainika kwamba wasichana kumi na nane kati ya 21 walioachiliwa na Boko Haram Alhamisi hii wana watoto, kwa mujibu wa vyombo vya usalama nchini Nigeria.

    Chini ya usimamizi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu,wasichana 21 waliotekwa nyara mwaka mmoja na nusu uliyopita kaskazini mwa Nigeria wameachiwa baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa serikali ya Nigeria na viongozi wa Boko Haram.

    Wasichana 21 waliotekwa na kundi la Boko Haram miaka miwili iliyopita, ambao waliachiliwa huru jana, wamekutana na makamu wa rais wa Nigeria Yemi Osinbajo.

    Bw Osinbajo amesema wasichana wote wamo buheri wa afya.

    Serikali ya Nigeria imekanusha taarifa kuwa wasichana hao waliachiliwa katika kubadilishana na maafisa wa Boko Haram waliokamatwa na vyombo vya usalama vya Nigeria.

    viongozi waandamizi wa Boko Haram walikamatwa katika kituo cha polisi cha kukagua magari karibu na mpaka na Cameroon, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako