• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 12-Novemba 18)

  (GMT+08:00) 2016-11-18 18:38:21

  Shinzo Abe akutana na Rais mteule wa Marekani Donald Trump

  Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amekuwa kiongozi wa kwanza kukutana na Rais mteule wa Marekani Donald Trump na amesema ana imani kwamba wawili hao wanaweza kuaminiana.

  Abe ameeleza mkutano wa dakika 90 kati yake na Bw Trump katika jumba la Trump Tower, New York, kama wa uwazi na wa kirafiki.

  Mkutano huo ulikuwa wa kwanza wa ana kwa ana kati ya Trump na kiongozi wa nchi nyingine duniani tangu ashinde urais.

  Marekani na Japan zimekuwa washirika wakubwa tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, ambapo Marekani iliisaidia Japan kufufua tena uchumi wake.

  Mkutano huo inadaiwa ulipangwa baada ya Bw Abe kumpigia simuTrump kumpongeza kwa kushinda uchaguzi wa urais, na kisha akamtajia kwamba angepitia New York akielekea Peru kuhudhuria mkutano wa kibiashara kati ya Asia na nchi za Pasifiki.


  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako