• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 12-Novemba 18)

    (GMT+08:00) 2016-11-18 18:38:21

    Zaidi ya wapiganaji elfu moja, raia wa Chad wamejiondoa katika kundi la Boko Haram

    Zaidi ya wapiganaji elfu moja, raia wa Chad wamejiondoa katika kundi la Boko Haram linaloendesha harakati zake nchini Nigeria na nchi jirani, na kuamua kurejea nchini mwao, hayo ni kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa Ziwa Chad Dimouya Souapepe.

    Kwa mujibu wa Dimouya, wanamgambo hao waliojitenga na kundi la Boko Haram, wakiwemo wanawake na watoto, wamekua wakijisalimisha kwa viongozi kwa kipindi cha miezi miwili.

    Wanajihadi hao wa zamani hawatawekwa jela, lakini watasikilizwa na viongozi wa Chad kabla ya kujiunga na familia zao.

    Wakati huo huo, jenerali Tukur Buratai, Mkuu wa majeshi ya Nigeria, amesema kwamba 60% ya wapiganaji wa Boko Haram ni kutoka Nigeria.

    Jenerali Buratai alitoa taarifa hiyo katika mkutano wa hivi karibuni mjini Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria, akiwa pamoja na Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi, Mohammed Ibn Chambas.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako