• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 19-Novemba 25)

    (GMT+08:00) 2016-11-25 18:24:03

    Watu elfu 68 wapoteza makazi kutokana na operesheni za kuukomboa Mosul, Iraq

    Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imeripoti kuwa hadi kufikia jumapili iliyopita, Umoja wa Mataifa umeandikisha watu zaidi ya laki zaidi ya 6 waliopoteza makazi kutokana na operesheni za kuukomboa mji wa Mosul nchini Iraq.

    Msemaji wa umoja huo Bw Stephane Dujarric amesema, tathmini ya afya iliyofanywa katika kambi ya Zelikan, kaskazini mashariki mwa Mosul imeonesha kuwa msaada wa kisaikolojia unahitajika miongoni mwa familia zilizopoteza makazi.

    Na kwingineko Polisi nchini Syria wamesema shambulizi la mizinga dhidi ya shule moja huko Aleppo, kaskazini mwa Syria limesababisha vifo vya wanafunzi 7 na wanafunzi wengine 19 na mwalimu mmoja wa kike kujeruhiwa.

    Polisi pia wamesema, wapiganaji mashariki mwa Aleppo wameshambulia maeneo mengi ikiwemo shule na hospitali katika eneo linalodhibitiwa na jeshi la serikali. Mbali na vifo na majeruhi kwenye shule hiyo, shambulizi hilo pia limesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 12 kujeruhiwa.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako