• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 26-Desemba 2)

    (GMT+08:00) 2016-12-02 20:11:26

    Fidel Castro, afariki akiwa na umri wa miaka 90

    Fidel Castro, kiongozi wa zamani wa Cuba aliyeongoza mapinduzi ya Kikomunisti, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, kakake Raul Castro ametangaza.

    Akitoa tangazo la kifo cha kakake, Rais Castro, aliyeonekana kuhuzunika sana, aliambia taifa kwenye tangazo la moja kwa moja kupitia runinga usiku kwamba Fidel Castro alikuwa amefariki na mwili wake umechomwa Jumamosi.

    Serikali imetangaza siku tisa za maombolezo ya kitaifa.

    Fidel Castro alitawala Cuba kama taifa la chama kimoja kwa karibu miaka 50 kabla ya kakake Raul kuchukua hatamu 2008.

    Mwakilishi maalumu wa rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni makamu wa rais wa China Bw. Li Yuanchao amekwenda Cuba kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Fidel Castro.

    Wakati wa utawala wake, alisaidia sana mataifa ya Afrika, hawa makundi yaliyokuwa yakipigania uhuru Angola na Msumbiji.

    Aidha, alikuwa akituma usaidizi wa matabibu na wataalamu, karibuni zaidi ikiwa nchini Sierra Leone wakati wa mlipuko wa Ebola..

    Katika miaka ya 1970 na 80, maelfu ya madaktari na walimu walikwenda Afrika na idadi sawa ya askari wa Cuba walipelekwa huko kuingilia kati migogoro na wakala wa vita baridi hasa nchini Angola.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako