• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 26-Desemba 2)

    (GMT+08:00) 2016-12-02 20:11:26

    Korea Kaskazini yasema itachukua hatua madhubuti za kujihami dhidi ya azimio jipya la Umoja wa Mataifa

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini amesema nchi hiyo itachukua hatua madhubuti za kujihami, ili kukabiliana na azimio jipya la Umoja wa Mataifa la kuiwekea vikwazo.

    Amesema majaribio ya nyuklia yaliyofanywa mwezi Septemba yameonyesha nia thabiti ya watu na jeshi la Korea Kaskazini kujibu uvamizi wowote, na Korea Kaskazini itaendelea kufuata njia yake ya kuendeleza silaha za nyuklia bila kujali hatua zinazochukuliwa na serikali ya Marekani.

    Baada ya kutolwa kwa azimio hilo la Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya pia unafikiria kuongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China inashikilia msimamo wa kuunga mkono kuondoa silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea, na inasisitiza kuwa azimio hilo la Umoja wa Mataifa linapaswa kutekelezwa kikamilifu kwa njia yenye uwiano.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako