• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Disemba 3-9)

  (GMT+08:00) 2016-12-09 22:02:10

  Wabunge wapiga kura kumfuta rais wa Korea Kusini Park Geun-hye

  Wabunge nchini Korea Kusini wamepiga kura kumuondoa madarakani Rais wa Park Geun-hye.

  Hoja hiyo imepitishwa na wabunge 234 dhidi ya 56.

  Maelfu ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Seoul wakitaka Bi Park aondolewe madarakani.

  Hatua hiyo itamlazimisha Bi Park kung'atuka kwa muda huku Mahakama ya Kikatiba ikiamua iwapo ataondolewa kabisa kutoka wadhifa huo wa urais.

  Suala kuu limekuwa ni uhusiano kati ya Bi Park na msiri wake mkuu Choi Soon-sil, ambaye anadaiwa kutumia uhusiano huo kujizolea ushawishi nchini humo.

  Viongozi wa mashtaka wanasema Bi Park alikuwa na "mchango mkubwa" katika visa kadha vya ufisadi, tuhuma ambazo amezikanusha.

  Aidha, alikataa wito wa kumtaka ajiuzulu akisema uamuzi huo aliuachia bunge.

  Bunge la Korea Kusini lilianzisha hoja hiyo Alhamisi, ambapo iilihitaji kuungwa mkono na angalau theluthi mbili ya wabunge ndipo kupitishwa.

  Wachanganuzi walikuwa wanasema hilo lingekuwa jambo ngumu.

   

  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako