• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Disemba 3-9)

    (GMT+08:00) 2016-12-09 22:02:10

    Waziri mkuu wa Italia Renzi awasilisha ombi la kujiuzulu

    Waziri mkuu wa Italia Bw Matteo Renzi amewasilisha barua ya kujiuzulu baada ya bajeti ya mwaka 2017 kuidhinishwa na baraza la seneti.

    Bw Renzi amekabidhi barua ya kujiuzulu kwa Rais Sergio Mattarella wa Italia, siku tatu baada ya kushindwa kwenye upigaji kura za maoni uliofanyika Jumapili kuhusu marekebisho ya katiba. Rais Sergio alimtaka Renzi aendelee kubaki madarakani hadi bajeti itakapopitishwa.

    Rais wa Italia atafanya mazungumzo na viogozi wa vyama vyote nchini ili kumteua waziri mkuu mpya na kuunda serikali mpya.

    Katibu mkuu katika ofisi ya rais wa Italia Bw Ugo Zampetti amesema kwamba baraza la mawaziri linaloongozwa na Bw Renzi litaendelea na kazi za utawala.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako