• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Disemba 3-9)

    (GMT+08:00) 2016-12-09 22:02:10

    Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Indonesia yafikia 97

    Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoa wa Aceh, magharibi mwa Indonesia imefikia 97 huku wengine zaidi ya 600 wakijeruhiwa.

    Ofisa habari wa masuala ya dharura katika mkoa huo Heni Nurmaini amesema, tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.4 kwenye kipimo cha Richter limeharibu nyumba zaidi ya 200, majengo ya maduka, shule, misikiti, na majengo mengine.

    Meja Jenerali Tatang Sulaiman wa kamanda ya Iskandar Muda amesema, operesheni ya uokoaji inaendelea, na kwamba tayari askari 1,050, polisi 900 na maofisa kutoka mamlaka ya kusimamia matukio ya dharura nchini humo wamepelekwa kwenye eneo la tukio.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako