• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Disemba 10-16)

    (GMT+08:00) 2016-12-16 18:43:15

    Kikundi cha pili cha waasi waondoka Aleppo

    Kikundi cha pili cha waasi na familia zao wameondoka Aleppo, mji wa kaskazini mwa Syria.

    Kikundi cha kwanza cha waasi na familia zao waliwasili kwenye eneo la Rashidien, kitongoji cha magharibi mwa Aleppo, kikiwa na watu zaidi ya elfu moja. Habari zinasema waasi na wakazi wa mashariki mwa Aleppo wataendelea kuondoka hadi kazi ya kuhama itakapokamilika.

    Inakadiriwa kuwa watu elfu 15 ikiwa ni pamoja na waasi elfu nne wataondoka kutoka eneo hilo, ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati ya Russia na Uturuki.

    Wataalamu wa Russia wamesema kuondoka kwa kundi la waasi kutoka mashariki mwa Aleppo, kutawezesha kuanza kwa operesheni za kibinadamu kwenye eneo hilo.

    Watu takriban elfu tatu wakiwemo mamia ya watoto wameanza kuokolewa kutoka maeneo yaliyokuwa yanashikiliwa na waasi huko Aleppo.

    Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu imesema watoa misaada kwa sasa wanachukua mamia ya watu kutoka maeneo mbalimbali na kuwapeleka sehemu salama zaidi.

    Mlolongo wa magari ya wagonjwa na magari ya abiria yamekuwa yakifanya kazi kubwa kusaidia kuwasogeza watu hao katika sehemu zinazoshikiliwa na serikali.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako