• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Disemba 24-30)

  (GMT+08:00) 2016-12-30 18:11:36

  China yataka waziri mkuu wa Japan kutafakari historia ya vita kuu vya pili

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bibi Hua Chunying amesema, wiki hii kwamba Japan inahitaji kutafakari historia yake kuhusu Vita vikuu vya Pili vya Dunia, na kuzingatia zaidi athari yake kwa nchi za Asia.

  Bibi Hua Chunying amesema, kitendo cha waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe kuzuru Pearl Harbor nchini Marekani na kutaka kufuta kabisa historia ya vita kuu ya pili ya dunia kuwa ni jambo lisilowezekana.

  Amesema bila ya maafikiano kati ya Japan na China na nchi nyingine za Asia, Japan haitaweza kufunga ukurasa huo wa historia

  Naye Profesa Peter Li wa chuo kikuu cha Houston, Marekani amesema, ziara ya waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe huko Pearl Harbour, Hawaii, haikuwa na haiwezi kuwa na maana mpaka pale atakapotambua uhalifu wa kivita uliofanywa na Japan.

  Prof. Peter amesema, kitendo cha Japan cha kukataa uhalifu wa kivita kimeonyeshwa wazi kwa nchi hiyo kukataa kuwatumia wanawake wa Asia kama "watumwa wa kingono" kwa askari wa Japan, na kukataa uhalifu wa kivita uliofanywa na Japan huko Nanking, China.

  Shinzo Abe aliandama na rais Barack Obama wa Marekani, kwenda kuhudhuria hafla ya kumbukumbu ya mauaji yaliyotokea Pearl Harbour mwaka 1941 baada ya Japan kufanya shambulizi la ghafla katika kambi ya jeshi, na kusababisha vifo vya maelfu ya askari wa jeshi la majini la Marekani.


  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako