• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Disemba 24-30)

    (GMT+08:00) 2016-12-30 18:11:36

    Wakimbizi wengi zaidi wa DRC waingia Zambia

    Wakimbizi wengi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wameingia Zambia kutokana na machafuko ya kisaisa nchini humo.

    Hali ya wasiwasi imeibuka baada ya Rais Joseph Kabila wa DRC kuendelea kuwepo madarakani licha ya muda wake kumalizika, na kusababisha vurugu za kisiasa nchini humo.

    Habari kutoka Zambia zinasema wakimbizi takribani 233 kutoka DRC wameingia kaskazini mwa Zambia.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Zambia Bw Chikeshe Mulenga amesema Zambia inaendelea kuwapokea wakimbizi wa DRC kupitia vituo mbalimbali vya forodha.

    Ofisi ya tume ya wakimbizi itashirikiana na idara za utekelezaji wa sheria, ili kuwakagua wakimbizi wote kabla ya kuwapeleka kwenye vituo vya wakimbizi.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako