• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Disemba 24-30)

    (GMT+08:00) 2016-12-30 18:11:36

    Kiongozi wa Boko Haram asema Bado kundi lake lipo msitu wa Sambisa

    Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, amerusha hewani Alhamisi hii video mpya ambapo anakanusha madai ya serikali ya Nigeria kwamba kundi la wanajihadi la Boko Haram lilitimuliwa katika msitu wa Sambisa, moja ya ngome yake ya mwisho kaskazini mwa nchi hiyo.

    Kwenye video hiyo Shekau anadai kwamba yeye na kundi lake wako salama, na hawatujatimuliwa mahali popote pale.

    Shekau alirekodiwa kwa video hiyo ya dakika ya 25 akiwa amezungukwa na wapiganaji waliojificha nyuso zao huku wakishikilia silaha.

    Wiki iliyopita, Rais wa Nigeria alibaini kuwa jeshi la Nigeria liliwatimu wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika ngome yao ya mwisho ya msitu Sambisa.

    Boko Haram imekua ikitekeleza mashambulizi ya kujitoa muhanga kaskazini-mashariki mwa Nigeria na nchi jirani ya Niger na Cameroon.

    Kulingana na makadirio, kundi la la Boko Haram liliua zaidi ya watu 15,000 wna kusababisha watu zaidi ya milioni mbili kuyahama makaazi yao kwa uasi unaodumu sasa miaka saba katika ukanda huo.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako