• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 7-Januari13)

    (GMT+08:00) 2017-01-13 18:26:42

    Uturuki na Russia zasaini makubaliano ya uratibu katika operesheni za anga nchini Syria

    Uturuki na Russia wiki hii zimesaini makubaliano ya kuanzisha utaratibu na uratibu kwa ajili ya usalama kwenye operesheni za anga nchini Syria.

    Makubaliano hayo yamefikiwa mjini Moscow yakilenga kuhakikisha usalama wa ndege katika operesheni.

    Uhusiano kati ya Uturuki na Russia umeboreshwa baada ya pande hizo mbili kushirikiana katika kuisaidia Syria kufikia makubaliano ya amani.

    Habari pia zinasema Russia imeanza mashambulizi dhidi ya kundi la IS karibu na eneo la al-Bab baada ya Uturuki kulalamika kuwa jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani halijasaidia katika mapambano hayo.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako