• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 7-Januari13)

    (GMT+08:00) 2017-01-13 18:26:42

    Nigeria kumpatia hifadhi rais Yahya Jammeh wa Gambia iwapo atajiuzulu.

    Bunge nchini Nigeria limeunga mkono mswada wa kumpatia hifadhi rais Yahya Jammeh wa Gambia iwapo atajiuzulu.

    Wabunge hao walitumia takriban nusu saa kujadili pendekezo hilo lililowasilishwa na Fani Zoro anayesimamia kamati ya wakimbizi bungeni.

    Jammeh Alipoteza uchaguzi mnamo mwezi Disemba ,lakini anataka matokeo ya kura hiyo kufutiliwa mbali.

    Bunge lilikuwa limefurika ,baada ya wawakilishi hao kutoka katika likizo yao ya mwaka uliopita.

    Baadhi ya wanachama hawakuunga mkono mapendekezo hayo wakisema kuwa wanamtambua rais Jammeh kuwa dikteta aliyechukua uongozi kupitia mapinduzi 1994 na kudai kuwa hatua kama hiyo itatuma ujumbe mbaya kwa viongozi wengine.

    Hatahivyo wabunge wengi waliunga mkono wakisema itakuwa njia ya kuzuia mgogoro zaidi wakisema kwamba iwapo ghasia zitaibuka nchini Gambia maafa yake yataathiri eneo lote la magharibi.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako