• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 14-Januari20)

  (GMT+08:00) 2017-01-20 18:31:17

   

  Rais mteule wa Gambia Adama Barrow aapishwa mjini Dakar Senegal

  Rais mteule wa Gambia Adama Barrow ameapishwa Alhamisi mjini Dakar Senegal katika ubalozi wa Gambia.

  Muda wa kuhudumu wa Rais Yahya Jammeh ulikuwa unakamilika siku hiyo lakini amekataa kuondoka madarakani akisema hakubali matokeo ya uchaguzi wa Desemba 2016 na hadi wakati tukienda hewani bado Jameh hakuwa ameachia mamlaka.

  Kumekuwa na hali ya taharuki katika mji mkuu Banjul huku raia wengi wakiondoka kuelekea Senegal.

  Wakili wa Jammeh pia ametorokea Senegal muda mfupi baada ya kumshauri Kiongozi huyo aachie mamlaka.

  Juhudi za viongozi wa jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS za kumshawishi Jammeh aondoke madarakani hazijafua dafu.

  Nigeria, Senegal na Ghana zinatuma wanajeshi na ndege za kivita nchini Gambia kumlazimisha Jammeh kung'atuka madarakani.Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Dlamini Zuma amewaambia raia wa Gambia kwamba Umoja huo pamoja na Umoja wa mataifa na Umoja wa Ulaya zinasimama nao wakati huu nchi hiyo ya Afrika Magharibi ikikabiliwa na hatari ya kutumbukia kwa mzozo baada ya Rais Yahya Jammeh kukataa kuachia madaraka.

  AU, EU na Umoja wa mataifa zimetoa taarifa ya pamoja kuunga mkono rais mpya Adama Barrow na watu wa Gambia.

  Zuma amemtaka Jammeh kuachia madaraka na kuheshimu katiba ya nchi hiyo.


  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako