• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 14-Januari20)

    (GMT+08:00) 2017-01-20 18:31:17

    Watu 30 wafariki baada ya theluji kuangukia hoteli Italia

    Watu 30 wamefariki nchini Italia baada ya barafu kuangukia hoteli moja nchini humo kufuatia tetemeko la ardhi.

    Waokoaji walifanya juhudi za usiku kucha kufika katika hoteli ya Rigopiano, huku wa kwanza akifika kwa kutumia ubao wa kutelezea juu ya theleji.

    Barafu iliosombwa na theluji hiyo ilifunga barabara za kuingia katika eneo hilo.

    Mtu mmoja amepatikana amefariki katika barafu hiyo. Wawili wamepatikana wakiwa hai lakini wengine wangi bado wamefukiwa chini ya theluji hiyo.

    Afisa mmoja amesema kuwa kuna watu wengi waliofariki katika hoteli hiyo.

    Eneo la milima katikati mwa Italia lilikabiliwa na msururu wa mitetemeko ya ardhi siku ya Jumatano pamoja na mitetemeko mingine usiku kucha.

    Mitetemeko hiyo ya ardhi imesababisha maafa mengi kutokana na kimbunga cha hivi majuzi ambacho kiliangusha miti ya stima mbali na kufunga barabara zinazoelekea vijijini.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako