• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 14-Januari20)

    (GMT+08:00) 2017-01-20 18:31:17

    Jeshi la Uganda lawakamata waasi wa zamani wa DRC

    Jeshi la Uganda wiki hii limewakamata wapiganaji 101 wa kundi la zamani la waasi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo M23 wakati walipojaribu kurudi nchini mwao.

    Msemaji wa serikali ya Uganda Bw Ofwono Opondo amesema wapiganaji hao waliokimbilia magharibi mwa Uganda mwaka 2013 baada ya kushindwa katika nchi yao walikamatwa walipokuwa njiani ya kurudi mashariki mwa DRC.

    Kwa sasa wako kizuizini kwenye kambi ya jeshi ya Makenke huko Mbarara.

    Bw. Ofwono amesema, kukamatwa kwao kunafuatia wapiganaji 40 wa zamani kufanikiwa kurudi DRC katika wiki iliyopita.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako