• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 14-Januari20)

    (GMT+08:00) 2017-01-20 18:31:17

    Watu 44 wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga Gao nchini Mali

    Watu 44 waliuawa Jumatano katika shambulizi la kujitoa mhanga katika mji wa Gao nchini Mali.

    Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amewaua watu wasiopungua 44 ikiwa ni pamoja na waasi wa zamani na wapiganaji wa makundi wanaounga mkono serikali mjini Gao kaskazini mwa Mali.

    Mlipuko huo ulitokea umbali wa mita 500 kutoka uwanja wa ndege ambapo mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyekua katika gari aliingia kambini na kujilipua.

    Watu wengi waliojeruhiwa walisafirishwa katika hospitali ya mjini Gao na kulindwa na askari. Serikali ya Mali imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

    Shambulio hilo linatokea wiki mmoja baada ya rais wa Ufaransa Francois Hollande kuzuru kambi hiyo ya mjini Gao ambapo maelfu ya askari wa Ufaransa walikuwepo.

    Wakati huo huo rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita amewataka wananchi wa Mali kushikamana na kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kukabiliana na mashambulizi kama hayo.

    Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo, na polisi ya amli imeanzisha uchunguzi.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako