• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Machi-31 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-31 20:06:38
    Waziri wa fedha wa Afrika Kusini afutwa kazi

    Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amemfuta kazi waziri wake wa fedha Pravin Gordhan baada ya majuma kadhaa ya kuenea kwa uvumi uliotikisa masoko ya nchi hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na ikulu wa Pretoria, imesema kuwa nafasi ya Gordhan sasa itachukuliwa na Mulusi Gigaba.

    Mapema wiki hii Gordhan aliamriwa kurudi nyumbani kutoka London alipokwenda kwa ziara ya kikazi, baada ya kutuhumiwa kuwa alikua akipanga njama za kuipindua serikali iliyopo madarakani.

    Kwenye taarifa yake rais Zuma amesema amewaagiza mawaziri wake wapya kufanya kazi usiku na mchana na wafanyakazi wao kuhakikisha wanaleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi ili kutumiza ahadi yake ya maisha bora kwa raia wa Afrika Kusini.

    Rais Zuma na Gordhan kwa miezi sasa wamekuwa wakitofautiana kwenye baadhi ya maeneo hali iliyosababisha mgwanyiko hata ndani ya chama cha ANC ambapo kuna maofisa wa juu wanaounga mkono juhudi za Gordhan anayeaminiwa na wawekezaji na mataifa ya magharibi.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako