• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Machi-31 Machi)

  (GMT+08:00) 2017-03-31 20:06:38

  Uingereza yaanza rasmi mchakato wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya

  Uingereza wiki hii imeanza rasmi mchakato wa kihistoria wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, baada ya barua iliyosainiwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Theresa May kupelekwa kwa viongozi wa Umoja huo.

  Akizungumza katika bunge la nchi hiyo, Bi. May amesema hatua hiyo ni ya kihistoria na hakuna kurudi nyuma, na kitakachofuata ni kuingia makubaliano ya kijasiri ya kibiashara na Umoja wa Ulaya.

  Hatua hiyo imekuja karibu miezi tisa baada ya Uingereza kupiga kura ya kujitoa kwenye Umoja huo kwa asilimia 51.9 ya kura za ndio dhidi ya asilimia 48.1 za hapana katika kura ya maoni iliyopigwa majira ya joto mwaka jana.

  Na wakati huohuo wabunge wa Scotland wiki hii walipiga kura kuunga mkono mswada wa kufanya tena upigaji kura za maoni kuhusu Scotland kujitenga na Uingereza, uliowasilishwa na Waziri mkuu Bibi Nicola Sturgeon, lakini mswada huo unatakiwa kuidhinishwa na serikali ya Uingereza kabla ya kutekelezwa. Kabla ya hapo, serikali ya Uingereza ilisema itaipinga Scotland kupiga kura za maoni kabla ya kujitoa rasmi kutoka Umoja wa Ulaya.

  Bibi Sturgeon amesema, watu wa Scotland wana haki ya kuchagua kati ya Brexit na kuwa nchi huru ya Ulaya.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako