• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Machi-31 Machi)

  (GMT+08:00) 2017-03-31 20:06:38

  Rais wa zamani Korea Kusini Park Geun-hye akamatwa

  Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani wiki chache zilizopita Park Geun-hye amekamatwa na kuzuiliwa kuhusiana na tuhuma za rusha ambazo zilichangia kutimuliwa kwake kutoka madarakani.

  Park mwenye umri wa miaka 65, alisafirishwa kwa gari hadi kwenye kituo cha kuwazuilia watuhumiwa wa uhalifu kusini mwa Seoul baada ya mahakama kuidhinisha kukamatwa kwake.

  Bi Park anatuhumiwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kudai pesa kwa lazima kutoka kwa kampuni kubwa kubwa, lakini amekanusha madai hayo.

  Rais huyo wa zamani aliomba radhi kwa umma wiki iliyopita, kabla ya kuhojiwa na maafisa wa mashtaka kwa saa 14.

  Waendeshaji mashtaka walisema Jumatatu kwamba wameamua kwamba ni vyema, kwa kufuata sheria na maadili nchini humo, kuomba kibali cha kumkamata.

  Walisema ushahidi, ambao unapatikana katika diski za kompyuta huenda ungeharibiwa iwapo Bi Park hangekamatwa.

  Bi Park anaweza kuzuiliwa kwa hadi siku 20 kabla ya kushtakiwa rasmi.

  Akipatikana na hatia, anaweza kufungwa kifungo cha hadi miaka 10 jela.

  Hwang Kyo-ahn, wambaye ni mwaminifu kwa Bi Park, kwa sasa ndiye kaimu rais na

  uchaguzi utafanyika tarehe 9 Mei.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako