• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Machi-31 Machi)

  (GMT+08:00) 2017-03-31 20:06:38

  Rais wa China kufanya ziara Finland na kukutana na Trump nchini Marekani

  Rais Xi Jinping wa China atafanya ziara ya kiserikali nchini Finland kabla ya kuelekea Florida, Marekani, kwa ajili ya mkutano wa marais wa China na Marekani utakaofanyika wiki ijayo.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lu Kang amesema, rais Xi atafanya ziara nchini Finland kuanzia tarehe 4 mpaka 6 mwezi ujao, kisha atakutana na rais Donald Trump wa Marekani huko Florida, Marekani, kuanzia tarehe 6 hadi 7 mwezi ujao.

  Lu amesema, ziara ya rais Xi nchini Finland itakuwa ni ziara yake ya kwanza kwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya kwa mwaka huu, na pia ni ziara ya kwanza kwa rais Xi kutembelea kaskazini mwa Ulaya kama rais wa China.

  Hii pia utakuwa ni mkutano wa kwanza kati ya rais Xi Jinping wa China na rais Donald Trump wa Marekani tangu rais Trump aingie madarakani mwezi Januari mwaka huu.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako