• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (22 Aprili-28 Aprili)

  (GMT+08:00) 2017-04-28 20:07:24

  Korea Kaskazini yaapa kuendelea kutengeneza silaha za nyuklia kwa ajili ya kujilinda

  Korea Kaskazini imesema itaendelea kuendeleza silaha za nyuklia kwa ajili ya kujilinda dhidi ya tishio la kijeshi kutoka Marekani.

  Makala iliyochapishwa kwenye gazeti la kila siku la nchini humo Rodong Sinmum imesema, hatua ya Marekani ya kupeleka meli ya kubeba silaha za nyuklia kwenye Peninsula ya Korea ni ya hatari. Makala hiyo imesema hatua hiyo ni ya usaliti dhidi ya Korea Kaskazini na ni kitendo cha hatari kinachoiweka peninsula hiyo kwenye hali tete zaidi.

  Hivi karibuni Korea Kaskazini imeongeza tuhuma zake kwa Marekani, ikiahidi kujibu kwa kutumia silaha za nyuklia wakati mvutano kwenye peninsula ya Korea ukiongezeka.

  Na huku hayo yakijiri Mamlaka ya rais Donald Trump imewaelezea maseneta wote 100 wa bunge la taifa hilo kuhusu tishio la Korea Kaskazini na kubaini mikakati ya kuishinikiza Pyongyang kupitia vikwazo vya kiuchumi na vile vya kidiplomasia.

  Lengo ni kuilazimu Korea Kaskazini kusitisha mpango wa makombora ya masafa marefu pampja na ule wa Kinyuklia.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako