• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (22 Aprili-28 Aprili)

  (GMT+08:00) 2017-04-28 20:07:24

  Mlipuko mkubwa watokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa mjini Damascus, Syria

  Mlipuko mkubwa umetokea katika eneo linalozunguka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus nchini Syria mapema leo.

  Vyombo vya habari nchini Russia vimesema, uwanja huo wa ndege ulishambuliwa katika mashambulizi matano ya anga yaliyofanywa na Israel, ambalo lengo lake halijajulikana. Uwanja huo una eneo la jeshi ambalo linahifadhi ndege za kivita na silaha.

  Iwapo itathibitika, hili halitakuwa shambulizi la kwanza kufanywa na jeshi la Israel dhidi ya Syria, kwa kuwa hivi karibuni, Israel imeongeza mashambulizi yake katika maeneo ya kijeshi nchini Syria, ikilenga kambi ya jeshi mkoani Qunaitera kusini mwa nchi hiyo wiki hii, na eneo la jeshi karibu na mji wa kale wa Palmyra mwezi uliopita.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako