• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (22 Aprili-28 Aprili)

  (GMT+08:00) 2017-04-28 20:07:24

  Rais Salva Kiir asitisha mkutano wake na maafisa wakuu wa jeshi

  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, amesitisha mpango wa kutembelea makao makuu ya jeshi jijini Juba. Mapigano yanaendelea kushuhudiwa nchini Sudan Kusini kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Riek Machar.

  Ripoti zinasema kuwa, rais Kiir alikuwa ameanza safari ya kwenda katika makao hayo makuu Kaskazini mwa jiji kuu la Juba lakini alipofika katikati ya safari yake, aliamua kusitisha ziara yake.

  Jeshi la Sudan Kusini limeendelea kushutumiwa na waangalizi wa Umoja wa Mataufa kwa kuendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya waasi na kusababisha maelfu ya raia w anchi hiyo kuyakimbia makwao.

  Umoja wa Mataifa unasema mwaka huu pekee, watu elfu 95 wamekimbia makwao kwa sababu ya mapigano yanayoendelea.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako