• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (12 Juni-18 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-16 19:02:39

    Shambulizi lauwa 25 mkahawani Mogadishu

    Watu 25 wameuawa baada ya kundi la kigaidi la Al Shabab kutekeleza shambulizi la bomu mjini Mogadishu nchini Somalia.

    Ripoti zinasema kuwa shambulizi hilo lilenga mkahawa maarufu katika mji huo mkuu.

    Gari dogo lililokuwa limetegwa bomu lilipuka lakini pia magaidi hao kuwapiga risasi baadhi ya watu waliokuwa ndani ya mkahawa huo.

    Abdi Bashir afisa wa usalama nchini humo amesema magaidi hao watano waliwazuia watu ndani na Mkahawa huo na kuanza kuwapiga risasi lakini wakalemewa.

    Aidha amesema kuwa walifanikiwa kudhibiti mkahawa huo na kuwauwa magaidi watano.

    Kundi la Al Shabab, limedai kuhusika na shambulizi hilo.

    Hii sio mara ya kwanza kwa mashambulizi kama haya kulenga mikahawa na maeneo mengine ya burudani nchini humo na kusababisha mauaji.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako