• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (12 Juni-18 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-16 19:02:39

    Bosco Ntaganda atoa ushahidi Mahakama ya ICC

    Aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la FPLC nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bosco Ntaganda, hatimaye ametoa ushahidi wa kujitetea katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC siku ya Jumatano.

    Ntaganda maarufu kama "The Terminator" amekuwa akikanusha madai kuwa aliwatumia watoto wadogo kama wapiganaji na kuwatumia wanawake na wasichana kama watumwa wa kingono.

    Kesi dhidi ya Ntanganda ilianza miaka miwili iliyopita mjini Hague nchini Uholanzi, alipofunguliwa mashtaka ya mauaji katika jimbo la Ituri yaliyotokea kati ya mwaka 2002 na 2003.

    Ntaganda mwenye umri wa miaka 43, amekanusha madai yote 13 ya uhalifu wa kivita na mengine matano ya ukiukwaji wa haki za binadamu, yaliyotekelezwa na waasi hao.

    Watu zaidi ya 60,000 walipoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao baada ya kuvamiwa na waasi hao.

    Kabla ya kufikishwa katika Mahakama ya ICC, Ntaganda alijisalimisha katika Ubalozi wa Marekani jijini Kigali nchini Rwanda mwaka 2013.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako