• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (12 Juni-18 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-16 19:02:39

    Watu 12 wafariki wafariki baada ya moto kuteketeza jengo refu London

    Watu 12 wamethibtiishwa kufariki baada ya moto mkubwa kuteketeza jengo refu mjini London, polisi wa jiji hilo wamesema.

    Wazima moto bado wanakabiliana na moto huo katika jumba la Grenfell Tower, ambapo walioshuhudia walisema kuwa watu walikwama ndani, wakiitisha msaada.

    Zaidi ya watu 50 wanatibiwa hospitalini.

    Kamishna wa wazima moto wa London Dany Cotton anasema wazima moto kadha walipata majeraha madogo.

    Walioshuhudia wanasema huenda kuna watu waliokwama kwenye jengo hilo, lililokuwa na nyumba 120 za makazi.

    Diwani wa Notting Dale Judith Blakeman, anayeishi hapo karibu, anasema kumekuwa na watu kati ya 400 na 600 ambao wamekuwa wakiishi katika jumba hilo.

    Meya wa London Sadiq Khan amesema wazimamoto walifanikiwa kufikia ghroofa ya 12 pekee.

    Habari nyingine zinasema, wizara ya mambo ya nje ya Morocco imethibitisha kuwa kulikuwa na wamorocco kadhaa kati ya watu waliokumbwa na moto huo, lakini hakuna raia wa Morocco aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako