• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (12 Juni-18 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-16 19:02:39

    Tanzania yapoteza matrilioni ya pesa kupitia usafirishaji mchanga wa madini

    Serikali ya Tanzania imepoteza takriban dola bilioni 84 za Marekani katika kipindi cha miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba.

    Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Tume iliyoundwa mwezi March mwaka huu na Rais John Magufuli.

    Ripoti hii imekuja siku chache baada ya Ripoti ya kwanza iliyojikita kueleza kiasi cha madini na fedha ambazo Tanzania hupoteza kutokana na usafirishaji wa mchanga wenye madini.

    Baada ya kutolewa kwa ripoti hiyo kampuni ya Barrick Gold Corporation, ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited, imesema ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha, ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

    Hayo ni kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

    Taarifa hiyo ilisema kuwa Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited, Prof John Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako