• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (10 Julai-14 Julai)

  (GMT+08:00) 2017-07-14 19:26:47

  Rais wa Somalia atoa mwito kwa bunge kuharakisha kazi ya kupitia katiba

  Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia amelitaka bunge la nchi hiyo kuharakisha mchakato wa mapitio ya katiba ya mpito inayotumiwa sasa na Somalia.

  Akihutubia mabaraza mawili ya bunge la nchi hiyo, Rais Farmajo amewataka wabunge kuwa mstari wa mbele kuhakikisha serikali inatoa huduma zenye lengo la kufikia mipango na maendeleo ya nchi.

  Pia amewataka kuhakikisha wanafanya kazi hiyo haraka na kwa maslahi ya taifa, na kuepuka maslahi binafsi, ya makundi au ya ukoo.

  Rais Farmajo pia ametaja baadhi ya malengo ya bunge, ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya kisiasa, kulainisha mgawanyo wa madaraka na majukumu kati ya serikali kuu na serikali za majiombo.

  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako