• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (10 Julai-14 Julai)

    (GMT+08:00) 2017-07-14 19:26:47

    Aliyekuwa rais wa Brazil Lula da Silva ahukumiwa miaka tisa jela

    Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Ignacio Lula da Silva, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa unusu jela miongoni mwa kesi tano za ulaji rushwa zinazomkabili.

    Lula aliondoka kutoka umaskini enzi za utoto wake na kuwa mmoja wa marais maarufu zaidi wa Brazil na kimataifa kwa sera zake za kijamii ambazo zilisaidia kuboresha maisha nchini humo.

    Lakini sasa mambo yamegeuka na kukutwa na hatia ya kukubali hongo ya zaidi ya dola milioni moja za malipo ya ghorofa ya mapumziko kwa ajili ya ukarabati wake kwa kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, iitwayo kwa kifupi OAS.

    Hukumu hii inakuja wakati ambapo mtawala Lula akiwa ametoa msimamo mkali kwamba ana mpango wa kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais mwakani .

    Kufuatia hukumu hiyo, rais huyo amekana mashtaka yote yanayomkabili kwa kudai kuwa hajafanya makosa yoyote kiasi cha kustahili hukumu hiyo, huku mawakili wanaomtetea wameapa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

    Wakati huo huo, kamati ya Bunge la Congress ya Brazil inajadili iwapo iiruhusu mahakama kuu kusikiliza kesi ya rushwa inayomhusisha Rais wa Brazil Michel Temer.

    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako