• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( 7 Agosti-11 Agosti)

  (GMT+08:00) 2017-08-11 18:20:21
  Trump asema Korea Kaskazini wanafaa kuwa na wasiwasi sana

  Rais wa Marekani Donald Trump wiki hii ameitahadharisha Korea Kaskazini kwamba inafaa kuwa na wasiwasi sana iwapo itatenda lolote kwa Marekani.

  Amesema utawala wa taifa hilo utakuwa shida kubwa "ambayo ni mataifa machache sana yaliyowahi kukumbana nayo" iwapo "hawatabadilika".

  Amesema hayo saa chache baada ya Korea Kaskazini kutangaza kwamba ina mpango wa kurusha makombora manne karibu na kisiwa cha Marekani cha Guam.

  Hali ya wasiwasi imeanza kuongezeka wiki za karibuni baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio makombora mawili ya kuruka kutoka bara moja hadi nyingine mwezi Julai.

  Umoja wa Mataifa hivi majuzi uliongeza vikwazo dhidi ya Pyongyang kutokana na mpango wake wa silaha za nyuklia lakini nayo Korea Kaskazini imepuuzilia mbali vitisho vya Marekani kama upuuzi.

  Korea Kaskazini ilisema Jumatano kwamba inapanga kurusha makombora ya masafa wa wastani na ya masafa marefu kuelekea kisiwa cha Guam, ambapo kuna kambi ya ndege za kivita za kuangusha mabomu za Marekani.

  Hata hivyo, kufikia sasa hakujakuwa na dalili zozote kwamba huenda kisiwa hicho cha Guam kikashambuliwa.

  Vikwazo hivyo vina lengo la kupunguza mapato kutoka kwa mauzo ya bidhaa nje ya Korea Kaskazini kwa theluthi moja.

  KCNA imesema Korea Kaskazini, ambayo imefanyia majaribio silaha za nyuklia mara tano, itajibu vikali na kwamba "Marekani italipia" kwa kuchangia kutunga vikwazo hivyo.

  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako