• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( 7 Agosti-11 Agosti)

    (GMT+08:00) 2017-08-11 18:20:21

    Mayai yenye sumu yaendelea kuzua wasiwasi barani Ulaya

    Mayai yenye sumu yaendelea kuzua wasiwasi barani Ulaya baada ya kubainika kwamba yana kemikali aina ya Fipronil, ambayo inaweza kudhuru figo, ini na tezi za shingoni za mwanadamu.

    Maafisa wakuu nchini Ubelgiji wamekiri kuwa, mnamo mwezi Juni, walifahamu mayai kutoka Uholanzi, huenda yalikuwa yameharibiwa na dawa ya kuuwa wadudu. Kashfa hii sasa imeigawa Ulaya na wasiwasi imeendelea kushuhudiwa katika nchi mbalimbali barani humo.

    Tani za mayai yalikamatwa katika nchi kadhaa za Ulaya, wakati ambapo watu kadhaa walikamatwa na kumekua kukifanyika operesheni ya kusaka mayai hayo tangu siku ya Alhamisi nchini Uholanzi na Ubelgiji.

    Siku ya Alhamisi jioni, Denmark ilitangaza kuwa tani ishirini za mayai yenye kemikali aina ya Fipronil yaliuzwa nchini humo.

    Mashamba 180 ya kufugia kuku nchini Uholanzi yamefungwa kwa muda siku za karibuni huku uchunguzi ukiendelea.

    Uchunguzi kuhusu ulaghai unaosababishwa na kuharibika kwa mamilioni ya mayai barani Ulaya kutokana na kemikali aina ya Fipronil, dawa inayotumiwa kwa kuua viroboto na kupe kwenye kuku, ya kampuni kubwa Ujerumani ya BASF inaendelea kuzua hali ya sintofahamu barani ulaya.

    Hayo yakijiri, maduka ya jumla barani Ulaya yamesitisha uuzaji wa mayai kutoka kwa vifurushi vya mayai ambavyo huenda viliambukizwa sumu hiyo.

    Hata hivyo, Aldi, ambao wana karibu maduka 4,000 nchini Ujerumani, ndio wa kwanza kusitisha uuzaji wa mayai kama tahadhari.

    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako