• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (16 Septemba-22 Septemba)

  (GMT+08:00) 2017-09-22 17:35:24

  Kimbunga Maria charindima Puerto Rico

  Kimbunga Maria kimekata umeme katika kisiwa chote cha Puerto Rico, chenye watu milioni 3.5.

  Baada ya kimbunga Maria kuipiga Puerto Rico, gavana ameamrisha watu kusalia manyumbani mwao kuanzia saa kumi na mbili jioni na hadi saa kumi na mbili asubuhi.

  Hi ni hatua ya kuwazuia watu kupata ajali kutokana na nyaya za umeme zilizoanguka na vifuzi vilivyo barabara za mji.

  Mkuu wa utoaji huduma za dharura Abner Gómez, alisema huduma za umeme zilikatika

  Kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema kuwa mafuriko makubwa yanaikumba nchi hyo.

  Mapema Bw Rossello alimuomba Rais Donald Trumo kukitangaza kisiwa hicho kuwa eneo la janga baada ya kimbunga kusababisha mafuriko makubwa na upepo unaotishia maisha.

  Alisema kuwa kuna uwezekano wa uharibivu mkuwa licha ya vitisho 500 kubuniwa kuwalinda watu.

  Kimbunga hicho tayari kimesababisha vifo vya watu 7 katika kisiwa cha Dominica ambacho kiliathiriwa vibaya siku ya Jumatatu


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako