• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (16 Septemba-22 Septemba)

  (GMT+08:00) 2017-09-22 17:35:24

  Airbus yazindua kituo cha kutengeneza ndege nchini China

  Kampuni ya Airbus wiki hii imezindua Kituo cha Kukamilisha na Ugavi wa ndege aina ya A330 mjini Tianjin, kaskazini mwa China, ikiwa ni kituo cha kwanza cha aina hiyo nje ya Ulaya.

  Mkurugenzi wa Airbus na rais wa Ndege za Kibiashara Fabrice Breiger amesema, kuzinduliwa kwa kituo hicho ni ishara ya hatua kubwa ya kimataifa ya kampuni hiyo na inaonyesha nia thabiti ya ushirikiano na China.

  Pia kampuni hiyo imekabidhi kwa Shirika la Ndege la Tianjin ndege ya kwanza aina ya A330 iliyokamilishwa kwa pamoja na wafanyakazi kutoka Ulaya na China.

  Airbus imesema, kituo cha Tianjin kitaajiri zaidi ya watu 250 na kitakuwa na uwezo wa kutoa ndege mbili kwa mwezi ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2019.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako